Tarehe 8 mwezi wa 3 kila mwaka huazimishwa siku ya wanawake duniani.Katika kuthamini mchango wao wa maendeleo leo...
tutangalia michango mbalimbali iliyofanywa na wanawake katika sekta muhimu ya sayansi na teknolojia ambapo mara nyingi hutawaliwa na wanaume. Nimekuletea wanawake kumi waliyofanya uvumbuzi wa vitu mbalimbali ambavyo vilibadilisha historia ya teknolojia duniani.
1. Florence Parpart. Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia hasa baada ya kuvumbuliwa na mwanamke.
2: Marie Van Brittan. Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera za CCTV mwaka 1969, ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork.
3.Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material yaliyotumika kutengeneza bullet proof, vikoti ambavyo huvaliwa kwa ajili ya kuzuia risasi isiingie mwilini.
4.Hedy Lamarr: Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyosaidia kuanzishwa kwa
WiFi na mfumo wa
GPS.
5.Josephene Cochrane. Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua machine ya kuoshea vyombo au dish washer ambazo alikuwa akiziuza mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda chake.
6.Letitia Gee. Mwaka 1899 Letitia Geer alivumbua bomba la sindano na kubadilisha historia ya sekta ya afya.
7.Dr Maria Telkes mwaka 1947 alijenga nyumba ya kwanza duniani yenye mfumo wa umeme wa jua au solar energy.
8. Maria Beasely Mwaka 1886 alibuni maboya ya kuogelea au life jackets baada ya kukithiri vifo vya baharini ni uvumbuzi uliyopongezwa na watu wengi na kumfanya Maria Beasely kuwa mwanasayansi mwenye jina kubwa.
9.Dr Shirley Jackson ni mwanafizikia aliyebuni nyaya au fiber cable zinazotumika leo hii kwenye mitandao ya simu, pia uvumbuzi wake mwingine uliyomjengea jina ni pamoja na machine ya fax, mfumo wa kusubirisha mtu kwenye simu au call waiting.
10.Ada Lovelace: Unaweza usiamini lakini computer programmer wa kwanza duniani ni mwanamke Ada Lovelace alikuwa mtu wa kwanza kubuni program mbalimbali za computer.