MTOTO WA MIAKA 11 ATUNIKIWA PhD
WAHITIMU, viongozi na wageni waliohudhuria Mahafali ya 32 ya Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro, waliingiwa na
simanzi wakati mtoto, Tamar Aaron Mbogho (11), alipojitokeza na kupokea
Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD), akimwakilisha mama yake Swai
Sophia Faustin ambaye alifariki dunia miezi sita kabla ya kufika siku ya
mahafali.