TOGETHER IN FUTURE COMMUNITY (TIFC)
TIFC ni kikundi kilicho anzishwa na vijana wanaopatikana wilayani Ilala Jijini Dar es salaam kikiwa na lengo kuu la kuhamasisha maendeleo maendeleo miongoni mwa wanakikundi na jamii kwa ujumla.
Malengo ya Kikundi
- Kuhamasisha vijana kukusanya nguvu na maarifa ili kujitolea katika kuleta Maendeleo.
- Kusaidiana katika Umoja wetu kwenye shida na raha.
- Kubuni na kuratibu shughuli mbalimbali za kijamii kwa lengo la kusaidia jamii husika.
- Kupokea misaada na michango mbalimbali kutoka kwa wadau tofauti kwa lengo la uendeshaji wa shughuli za kikundi.